Mtaa si kurahisi. Unaona wasee wako busy, wengine wanaingia job, wewe uko kwa stage ukihesabu fare ya kurudi kutoka job hunting. Ukiingia WhatsApp, kila mtu anaonekana ana-win. LinkedIn ni success stories tu za wasee. Lakini in reality? Raia mingi inapush Tu silently.
Unemployment si tu kukosa job. Ni kukosa peace pia. Ni kuanza kuquestion worth yako. Ni kuavoid family gatherings juu swali ni Ile ile, "Uliwai mboka?"
Lakini usijiweke chini morio. Joblessness haimaanishi wewe ni failure. System iko vile iko. Competition ni tough. Rai mingi umesoma hii nchi. Degree si guarantee tena.
So while unasaka mboka:
- jifunze vitu mpya
- Network
- Jaribu side hustles.
- Build mdogoo mdogoo
Na muhimu kuliko yote, usikubali pressure ya social media ikumalize. Watu wengi wanaonekana wako mbele, lakini kila mtu ako na race yake.
Siku moja kila kitu itaivana. Lakini hii githaa we hustle, piga mboka yoyote, jitume vile unaeza na usawai loose HOPE. Hi ndio kila kitu. Kama chonjo kaa rada. Mtaa ni ngumu, lakini story bado haijaisha. Nimeona mbogi ikiomoka kimchezo Tu, one by one. Majamaa walikua Tu wanakaa zabe wakiwa kajaba hapo na mafegi. Walikua wanapiga mboka zote wakiwa Tu na izo degree. Ngora, mkoko, kuhamisha, na vitu zingine mob. Haifai eti unakaa chini unafold mikono, Una frown. Jitumee jamaa, hakuna huruma kwa hii dunia. Saa zingine msee huitiaji helping hand, ukipata msee anakuokolea kimaisha, Nani anguka nayo.
Na pia usikubali kupoteza confidence yako. Hio ni kitu ya muhimu kwa hii game of life. Lazima ujitambue ndio wakutambue. Saa zingine itatake time but stay strong. Make sure kila siku yako umedishi Tu the maximum kivyovyote vile. Usiache vitu zikuweke down Sana. Kukua down Sana zingine ninkawaida but usikue Sana ama utanipata umelost. Kuna msee alisema, you win today, celebrate and tomorrow get back to work, you lose today, grieve today and tomorrow get back to work. TunaeA chukulia hii kama analogy ya kusema, ata kitu yoyote ikihappen make sure umeovr I haraka sababu ivyo ndio Life iko. Don't waste alot of time crying over spilt milk. When you point to the moon and look at the finger instead of the moon, you miss the beauty of all of it (bruce lee).
Inshallah
Loading comments...
Related Stories
Explore More Topics
No topics available at the moment