Chapter 9

Chapter 9
3 min read
0 reads

SURA YA 9: KITUONI

Asubuhi iliyofuata, nilikwenda kituo cha polisi cha Kilimani nikiwa na kadi ile ya ajabu mfukoni mwangu, pamoja na statement ya Brian niliyoipata kupitia advocate wake usiku uliopita.

Inspekta Wanjala alinipokea ofisini kwake — chumba kidogo chenye harufu ya karatasi za zamani na kahawa iliyopoa.

"Kaa," alisema, akinionyesha kiti. "Bwana Brian Otieno ametoa maelezo marefu kuhusu vitendo vyake. Amekutaja wewe kama mmoja wa waathirika wa moja kwa moja."

Nilimpa statement niliyokuwa nayo, pamoja na kadi ile ya ajabu niliyopewa na mama.

Wanjala aliisoma kadi kwa makini, uso wake ukibadilika kidogo. "Hii ni ya kutisha. Umeipata wapi?"

"Mama alipewa na mtu asiyejulikana jana, wakati mimi sikuwepo nyumbani."

"Tutaichunguza," alisema, akiiweka kwenye faili. "Kwa sasa, hebu tuzungumze kuhusu mikopo mitatu iliyofunguliwa kwa jina lako."

Tulizungumza kwa saa moja nzima, mimi nikieleza kila undani nilioukumbuka, Wanjala akiandika kila neno kwa makini.

"Kulingana na ushahidi huu na statement ya Bwana Otieno," alisema mwishowe, "tunaweza kuandaa ripoti ya kuthibitisha kwamba mikopo hiyo mitatu ilifunguliwa...

Want to support this author?

By unlocking the full story, you directly support local writers. You'll also be able to track your reads, and discover amazing content!

Chapter 9 - MKOPO WA KSH 13,000 | Soma