Chapter 2

Chapter 2
4 min read
0 reads

SURA YA 2: TABASAMU LA BRIAN

"John! Mzee wangu!" Brian alipiga kelele, akikimbia hatua mbili za mwisho kunifikia. Mkono wake mkubwa ulinishika bega kwa nguvu, kama kawaida yake.

Sikujibu haraka. Macho yangu bado yalikuwa yametoka kwa mwelekeo ambao ile sauti ya mwanamke ilikuwa imeninyima amani.

"Usimpe Brian hizo pesa."

"Uko sawa?" Brian aliniangalia kwa makini, tabasamu likipungua kidogo usoni mwake. "Unaonekana kama umeona kizuka."

Nilijikaza kutabasamu. "Niko sawa tu. Sikulala vizuri."

Ilikuwa uongo mwingine — wa pili siku hiyo, kabla hata jua halijachomoza kikamilifu.

Brian alinitazama sekunde moja zaidi kuliko ilivyokuwa lazima, kisha akatabasamu tena, pana zaidi. "Sawa basi. Twende. Nimekuletea mtu unayepaswa kumfahamu."

Ndipo nilipomwona.

Alikuwa amesimama kando ya duka dogo la vipodozi, akipanga bidhaa kwenye rafu, nywele zake zimefungwa nyuma kwa kitambaa cha rangi ya machungwa. Aliposikia sauti zetu, aligeuka.

Macho yake yalikutana na yangu kwa sekunde moja tu.

Kitu fulani ndani yangu kikasimama tuli.

"Huyu ni Aisha," Brian alisema, akinionyesha kwa mkono. "Anafanya kazi hapa dukani, lakini pia ana connections nzuri za wauzaji wa perfume kutoka Eastleigh. Yeye ndiye atakayetusaidia kupata bei nzuri ya stock."

"Habari," Aisha alisema, akinipa mkono wake. Mkono wake ulikuwa laini lakini imara.

"Habari," nilijibu, sauti yangu ikitoka nyororo kidogo kuliko nilivyotarajia.

Brian alicheka kwa sauti ndogo, kama vile alikuwa ameona kitu ambacho hakukusudia kukiona. "Sawa, waacheni mzungumze biashara kidogo," alisema, akinivuta pembeni.

Tulikaa kwenye benchi dogo nje ya duka. Brian alitoa daftari lake — moja...

Want to support this author?

By unlocking the full story, you directly support local writers. You'll also be able to track your reads, and discover amazing content!

Chapter 2 - MKOPO WA KSH 13,000 | Soma