Chapter 2: Niko KadiBaada ya ile drizzle night, kila kitu kwa plot ilianza kuonekana tofauti. Corridor haikuwa corridor tena — ilikuwa memory lane. Kila nikifungua mlango yangu, nafeel kama naingia stage ya series fulani.
Siku mbili zilipita bila drama. Tulikuwa normal. Ama at least tulijifanya normal.
Lakini tension ilikuwa iko hai.
Leo jioni nikampata kwa stairs. Alikuwa amevaa white top na zile jeggings zake black — zile zenye zilianza hii story. Nywele zimefungwa loose, perfume yake ikapita karibu nami kama reminder ya ile hug.
“Uko quiet sana siku hizi,” akasema akinishukia stair moja.
Nikacheka. “Mi? Wewe ndio umekuwa mysterious.”
Akashika railing, akaniangalia straight. Ile eye contact haikuwa ya jokes. Ilikuwa ile ya kupima...