Chapter One: Drizzle Ilianza NayoMiaka 2½ si mchezo kuishi plot moja na mtu halafu mko tu kwa “hi–bye” level. Huyo dem nilimzoea kama vile mtu anazoea background music — iko, unaisikia, but hujawai kaa chini ui-listen vizuri.
Anaitwa Njeri. (Sio jina yake real but wacha tuite hivo.)
Nilianza kumnotice kitambo. Si kwa ubaya, but naturally. Alikuwa na ile confidence ya quiet girls. Hatetemeki, hataki attention, but attention inamtafuta yenyewe. Jeggings zilikuwa uniform yake unofficial. Na zilikuwa zinamfit kama zilitengenezwa na destiny.
Lakini hatukuwahi cross line. Tulikuwa tu majirani civilized.
Mpaka ile jioni ya drizzle.
Ilikuwa kama saa moja jioni. Ka mvua ka Nairobi, si kubwa, si ndogo. Ile ya kufanya compound inuke harufu ya udongo fresh. Nilikuwa nimesimama kwa corridor niki-check simu, nikisubiria mvua...